Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ayataka mataifa tajiri kutimiza ahadi ya kufadhili miradi ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

Ban ayataka mataifa tajiri kutimiza ahadi ya kufadhili miradi ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuna changamoto katika kuchangisha bilioni 100 kwa mwaka fedha zitakazosaidia nchi zinazoendelea kupambana na madadiliko ya hali ya hewa.

Akiongea mjini Durban Ban amesema kwamba ufadhili ulioafikiwa mjini Cancun Mexico unaweza kuafikiwa kwa kujumuisha fedha kutoka sekta ya umma na zile za kibinafsi. Ban ameongeza kuwa usaidizi wa kiteknolojia na kifedha ndiyo masuala muhimu yatakayosaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa hata wakati huu wa hali mbaya ya uchumi duniani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)