Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasafirisha wahamiaji kutoka Libya

IOM yasafirisha wahamiaji kutoka Libya

Msafara wa malori kwenye Shughuli iliyofadhiliwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ya kuwasafirisha wahamiaji 840 kutoka Afrika sasa umeingia nchini Chad baada ya kusafiri kutoka mji ulio kusini mwa Libya wa Sebha.

Wahamiaji hao wengi wakiwa ni kutoka nchini Chad waliwasili kwenye mji wa Zouarke ambapo wafanyikaji wa IOM waliwapokea na kuwahudumia. Hiyo ndiyo shughuli ya pili ya kusafirisha wahamiaji kutoka mji wa Sebha tangu ile ya mwezi Oktoba ambapo wahamiaji 1220 kutoka nchi tofauti walisaidiwa. Jumbe Omari Jumbe wa IOM amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali hii.

 SAUTI YA JUMBE