Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya nusu ya vijiji nchini Niger vyakabiliwa na uhaba wa chakula

Zaidi ya nusu ya vijiji nchini Niger vyakabiliwa na uhaba wa chakula

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa taifa la Niger linakabiliwa na wakati mgumu kwenye sekta ya kilimo hali inayohatarisha usalama wa chakula nchini humo. Kwa sasa utapiamlo nchini Niger umefikia asilimia 13 kulingana na utafiti uliofanywa mwezi Oktoba.

Serikali inasema kuwa bado imeshindwa kukusanya tani 520 za nafaka na tani kumi za chakula cha ng’ombe kwenye kampeni yake. OCHA inasema kuwa mzozo uliokuwa nchini Libya na uliosababisha kurejea nyumbani raia 200,000 wa Niger umechangia katika kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)