Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watumia uvumbuzi katika kuelewa masuala ya uchumi duniani

UM watumia uvumbuzi katika kuelewa masuala ya uchumi duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Global Pulse ambao ni ufumbuzi kutoka kwa ofisi ya Katibu Mkuu ulio na lengo la kuvumbua teknolojia mpya kwa maendeleo ya kimataifa.

Uvumbuzi huo unawaleta pamoja wataalamu kutoka nje na ndani ya Umoja wa Mataifa ili kujifunnza jinsi teknolojia za kisasa zinaweza kuwasaidia watoa maamuzi hasa wakati huu wa changamoto nyingi za kiuchumi.