Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yasherehekea miaka 40 ya mkataba wa utamaduni

UNESCO yasherehekea miaka 40 ya mkataba wa utamaduni

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova ameongoza maadhimisho ya miaka 40 ya mkataba kuhusu utunzi wa maeneo ya kitamaduni duniani uliotiwa sahihi na wanachama wa UNESCO mwaka 1972.

Bokova amesema kuwa utamaduni umeathiriwa na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya masuala ya kijamii na kuongeza kuwa utamaduni ni kama kitambulisho cha watu. Flora Nducha anaripoti.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)