Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa nyuklia ni muhimu kwa mataifa yote:IAEA

Usalama wa nyuklia ni muhimu kwa mataifa yote:IAEA

Suala la kuhakikisha malighafi ya nyuklia halianguki kwa wasiostahili kuwa nayo ni muhimu sana kwa mataifa yote amesema mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA.

Yukiya Amano ameliambia Baraza Kuu hii leo kwamba kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, shirika la IAEA limepanua wigo wa mipango ya usalama wa nyuklia.

Bwana Amano amesema sasa hivi kuna nchi 113 ambazo zinashiriki katika mpango wa mtandao wa kudhibiti nyuklia wa shirika hilo ITDB na idadi inaendelea kuongezeka.

Amesema hadi kufikia Juni 2011 matukio 172 yameripotiwa kwenye mtandao wao, 14 kati ya hayo yanahusisha umiliki haramu au majaribio ya kutaka kuuza au kusafirisha kinyemela malighafi za nyuklia. Ameongeza kuwa matukio mengine 32 ni ya wizi au upotevu wa nyuklia au malighazi za nyuklia.