Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yajiunga na kampeni ya watu bilioni 7 kuonyesha fursa na changamoto

UNEP yajiunga na kampeni ya watu bilioni 7 kuonyesha fursa na changamoto

Idadi ya watu duniani itafikia bilioni 7 hapo Oktoba 31 mwaka huu na kuleta changamoto ya kuhakikisha maendeleo endelevu na usawa katika kugawana rasilimali kukidhi idadi hiyo ya watu. Kwa kulitambua hilo shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP leo limejiunga na kampeni ya kuchukua hatua kukidhi matakwa ya watu bilioni 7 kwa kuwachagiza watu, serikali, wafanyabiashara na mashirika kuchukua mtazamo na hatua muafaka za kuifanya dunia kuwa mahala bora kwa ajili ya watu bilioni 7.

Kampeni hiyo ambayo inaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA ina lengo la kutumia kufikia idadi hiyo ya watu kupigia upatu ushirikiano wa kimataifa kuhusu masuala ya afya, mazingira, umasikini na usawa, ukuaji wa miji na masuala mengine muhimu kwa ajili ya maisha ya watu hao.