Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Soko la nafaka linatarajiwa kusalia kuwa juu licha ya ongezeko la uzalishaji:FAO

Soko la nafaka linatarajiwa kusalia kuwa juu licha ya ongezeko la uzalishaji:FAO

Licha ya kuongezeka kwa matarajio ya uzalishaji, soko la dunia la nafaka linatarajiwa kusalia kwa la juu kwa mwaka 2011/2012 limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO.

Ripoti ya FAO ya matarajio ya hali ya mazao kwa robo ya mwaka inaonyesha kuwa uzalishaji wa nafaka duniani utafikia tan milioni 2301 katika msimu huu ikiwa ni asilimia tatu zaidi ya mwaka 2010/2011. Na hii ni tani milioni 3 zaidi ya matarajio ya FAO, sababu kubwa ikiwa ni kuimarika kwa uzalishaji wa mazao ya ngano na mpunga. FAO inasema kwa ujumla kuna ongezeko la asilimia 4.6 la zalishaji wa ngano duniani, asilimia 3 ya mavuno ya mpunga na asilimia 2.1 ya nafaka zingine.