Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua mradi wa kutumia simu za mkononi kusaidia masikini kwa chakula Ivory Coast

UM umezindua mradi wa kutumia simu za mkononi kusaidia masikini kwa chakula Ivory Coast

Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa majaribio ambayo inatumia teknolojia ya simu za mkononi kutuma fedha za kusaidia maelfu ya watu masikini ambao waliathirika vibaya na machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast kununua chakula.

Zaidi ya familia 10,000 kwenye wilaya za Abobo na Yopougon mjini Abuja zitapata ujmbe kwenye simu zao za mkononi ukiwajulisha kuhusu fedha walizotumiwa na kuwawezesha kuchukua fedha hizo kwenye vituo vya fedha vya kampuni za mtandao wa simu wa MTN. Hayo yameelezwa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP lililozindua mradi huo. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)