Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya utalii ni muhimu katika kupunguza umaskini:UM

Sekta ya utalii ni muhimu katika kupunguza umaskini:UM

Maafisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa wamesisitiza umuhimu wa sekta ya utalii katika kupunguza umaskini wakati kunapoadhimishwa siku ya utalii duniani.

Akitoa ujumbe kwenye siku hii katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa sekta ya utalii ina umuhimu hususan wakati wa kipindi cha uchumi mbaya na pia inachangia kupunguza nafasi iliyopo kati ya matajiri na wale maskini. Naye katibu mkuu wa shirika la utalii la Umoja wa Mataifa Taleb Rifai amesema kuwa utalii una umuhimu mkubwa ukichangia katika utunzi wa tamaduni na sehemu za kitamaduni.