Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kuanza ziara ya kutembelea mataifa manne

Ban kuanza ziara ya kutembelea mataifa manne

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anajiandaa kwa ziara ya kuyambelea mataifa manne itakayomchukua kuanzia Australia hadi katika visiwa na Solomon ambako anatazamiwa kutilia uzito masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika ziara hiyo inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa juma hili, Ban mbali ya kuzitembelea nchi hizo mbili, lakini pia atatembelea New Zealand,na Kiribati .

Akijadilia ziara yake hiyo, Ban alitaja maeneo matatu ambayo anatazamiwa kuyapa uzito ikiwemo pia kuweka ulewa wa karibu kuhusiana na chombo cha kung’amua na mapema majanga ya kimazingira kilichowekwa katika bahari ya Pacific.

Pia anatazamiwa kuhudhuria kongamano maalumu litalokayojumuisha eneo ya pwani ya Pacific na hivyo kufanya Katibu Mkuu wa kwanza kuhudhuria mkutano huo.