Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kujadili uhusiano uliopo kati ya vijana na sekta za kibinafsi waandaliwa

Mkutano wa kujadili uhusiano uliopo kati ya vijana na sekta za kibinafsi waandaliwa

Idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya uchumi na kijamii kwa ushirikiano na ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano imeandaa mkutano wa siku moja kujadili uhusiano uliopo kati ya vijana na sekta za kibinafsi na jinsi vijana wanavyoshiriki kusaidia kwenye maendeleo kwa umma.

Mkutano huo utawaleta pamoja wafadhili , wanaharakati vijana na watu kutoka sekta za kibinafsi. Moniqe Coleman ambaye ni bingwa wa wa vijana alihudhuria mkutano huo na amezungumza na Julie Walker wa idhaa hii.