Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa Darfur hawawezi kusubiri zaidi kupata maji, na matumaini yapo:UM

Wananchi wa Darfur hawawezi kusubiri zaidi kupata maji, na matumaini yapo:UM

Makala hii maalumu inahusu jitihada za Umoja wa Mataifa, jumuiya ya kimataifa, serikali ya Sudan na wadau wengine wa maendeleo kuisaidia Sudan na hasa jimbo la Darfur kutatua tatizo la maji.

Jimbo hilo mbali ya kughubikwa na machafuko yaliyokatili maisha ya watu zaidi ya milioni moja na kuwafungisha wengine kwa mamilioni virago, uhaba wa maji umedhidisha adha na kuna hofu utaweza kutia dosari juhudi za kuleta amani ya kudumu amesema mkuu wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID profesa Ibrahim Gambari.

Kwa kulitambua hilo UNAMID kwa ushirikiano na serikali ya Sudan wiki iliyopita waliitisha mkutano mkubwa na kutoa ombo la msaada wa takribani dola bilioni moja kusaidia kumaliza tatizo la maji Darfur.

Wito umeiitikiwa na wahisani mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Bwana Emmanuel Mollel mkuu wa mradi wa maji na mazingira wa UNAMID anasema ukosefu wa maji ni suala ambalo watu wa Darfur hawawezi kusubiri tena. Akizungumza na Flora Nducha anatanabahi matumaini waliyonayo baada ya mkutano

(MAHOJIANO NA EMMANUEL MOLLEL)