UNRWA yaandaa watoto wa Gaza kuweka rekodi

29 Juni 2011

Zaidi ya wanafunzi 3000 kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Kipalestina la UNRWA kwenywe ukanda wa Gaza wanatarajiwa kuvunja rekodi nne wakati wa sehemu ya mshindano ya msimu wa joto yanayoandaliwa na shirika hilo.

Rekodi ya idadi kubwa zaidi ya watu wanaoruka kwa kutumia miavuli mikubwa kutoka ardhini iliwekwa na watu 1,547. Msemaji wa UNRWA Chris Gunnes anasema kuwa wataongeza watu mara mbili zaidi kwenye rekodi hiyo.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter