UM watumia kombe la dunia la wanawake kuanzisha kampeni ya kuwawezesha wanawake

28 Juni 2011

Mnamo wakati miamba ya soka ikichuana huko Ujerumani kwenye fainali za kombe la dunia kwa wanawake, shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP linatumia michuano hiyo kuanzisha kampeni yenye shabaya ya kuwewezesha wanawake kuchukua nafasi za juu kwenye maisha ya kila siku.

Kampeni hiyo ambayo inamulika kwa karibu yale yaliyomo kwenye malengo ya maendeleo ya milenia, inaweka msukomo kwa kutaka wanawake wanaendelea kuchanua tangu wakiwa shuleni hadi kwenye maeneo ya kazi. Michuano ya kombe la dunia kwa wanawake ilianza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki na inatazamiwa kudumu hadi July 17 nchini huko Berlin, Ujerumani.

Na kwa kutumia kombe hili la Dunia UNDP inasema kwamba ujembe huo utawafikia mamilioni ya wananchi duniani kote.Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, wanawake duniani kote wanaendelea kusalia wenye kipato cha chini licha kwamba wanashika nafasi za juu kwenye uchangiaji wa pato la uchumi wa nchi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter