Pillay aomba usaidizi wa kimataifa kwa waathiriwa wa mateso

28 Juni 2011

Mkuu wa tume ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametoa wito wa kutolewa usaidizi wa kimataifa kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia waathiriwa wa mateso unaotoa usaidizi kwa zaidi ya miradi 65 barani Afrika, Asia ya kati, Amerika Kusini na Mashariki mwa Ulaya na kwa maelfu ya waathiriwa wengine kila mwaka.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho yaliyoandaliwa na waathiriwa wa mateso kuadhimisha miaka 30 ya mfuko huo  Pillay amesema kuwa wanachama ambao bado hawajatoa mchango wao kwenye mfuko huo watoe ili waathiriwa zaidi wa mateso wapate kufaidika.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud