Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la salama lapendekeza muhula wa pili kwa Ban

Baraza la salama lapendekeza muhula wa pili kwa Ban

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limependekeza kwamba baraza kuu la Umoja wa Mataifa limteuwe Katibu Mkuu wa sasa Ban Ki-moon kwa muhula wa pili wa miaka mitano kuuongoza Umoja wa Mataifa.

Ban ambaye ni raia wa Korea Kusini aliteuliwa kuwa Katibu mkuu wa nane wa Umoja wa Mataifa Januari 2007.

Balozi Noel Nelson Messone wa Gabon ni rais wa baraza la usalama kwa mwezi huu wa June akitangaza hatua ya baraza la usalama amesema

(SAUTI YA NELSON MESSONE)

“Baraza la usalama baada ya kutafakari suala la kupendekeza uteuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , linapendekeza kwa baraza kuu la UM kwamba bwana Ban Ki-moon ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa muhula wa pili kuanzia Januari mosi 2012 hadi Desemba 31 mwaka 2016.”

Akionyesha furaha yake kwa pendekezo hilo Ban ambaye yuko ziarani nchini Brazili amesema

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Baraza kuu la Umoja wa mataifaifa linatarajiwa kuidhinisha uteuzi wa Katibu Mkuu Jumanne ijayo.