Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaelezea maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani

UNHCR yaelezea maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limetoa vipaumbele vitavyozingatiwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambayo hufanyika kila mwaka Juni 20.

Lakini maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika katika wakati ambapo kunasherekewa kutimia mwaka wa 60 tangu kutolewa tamko la umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu.

UNHCR inatazamiwa kutoa taarifa maalumu wakati wa maadhimisho hayo kuelezea mwenendo na hali ya wakimbizi duniani kote. Ama kamishna mkuu wa haki za binadamu Guterres atatazamiwa kutembelea Tunisia na kuzulu kisiwa cha Lampedusa kilichoko Italy kama sehemu ya maadhimisho hayo.

Naye balozi wa hisani Angelina Jolie leo anatazamiwa kujitokeza hadharani kwa ajili ya kuanzisha kampeni inayohimiza ulimwengu kuwasaidia wakimbizi