Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la saratani laongezeka barani Afrika

Tatizo la saratani laongezeka barani Afrika

Saratani imekuwa ni tatizo kubwa kwa nchi zinazoendelea hivi sasa. Shirika la afya duniani WHO linakadiria kwamba zaidi ya watu milioni 10 waliopimwa na kujulikana kuwa wana saratani wanatoka wako katika nchi zinazoendelea.

Nchi nyingi kati ya hizo hazina fedha za kutosha na vifaa vinavyohitajika , hivyo shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA linatoa wataalamu wake kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na ugonjwa huo wa saratani.

Saratani mara nyingi imekuwa ikionekana kama ugonjwa wa nchi tajiri lakini ukweli ni kwamba karibu robo tatu ya vifo vyote vitokanavyo na saratani vinatokea nchi zinazoendelea, idadi ambayo ni sawa na ndege kubwa aina ya Jumbo Jet kuanguka kila saa na idadi inaendelea kuongezeka.

Afrika haijasalizwa na ugonjwa huo, na Nigeria ikiwa ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika inabeba sehemu kubwa ya tatizo hilo. Katika nchi hizi zinazoendelea ukosefu kwa njia ya kuzuia, kupimwa, na vifaa vya matibabu kunamaanisha kwamba mamilioni ya watu wanakufa , ambao maisha yao yangeweza kuokolewa kama ingekuwa ni kwenye nchi zilizoendelea.

Woga na watu kuchelewa kupimwa kunachangia sana idadi kubwa ya watu kupoteza maisha kwa sababu wanakuwa wamechelewa sana, lakini hata wakijua na kwenda hospitali wengi hawawezi kumudu gharama za matibabu.