Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapendeleo ya kijinsia kwa watoto wa kiume yasababisha kutelekezwa, talaka na hata vifo:UM

Mapendeleo ya kijinsia kwa watoto wa kiume yasababisha kutelekezwa, talaka na hata vifo:UM

Shinikizo za kuwataka wanawake kuzaa watoto wa kiume zimetajwa kama baadhi ya masuala yanayochangia kuwepo kwa ubaguzi na dhuluma dhidi ya wanawake . Hii ni kulingana na ripori ya mashirika matano ya Umoja wa Mataifa inayosema kuwa kuwapendelea watoto wa kiume kunaweza kukachangia kuwepo kwa dhuluma, kutelekezwa, talaka au mara nyingine vifo kwa wanawake wanaozaa wasichana.

Suala hili linatajwa kukita mizizi kusini , mashariki na kati kati mwa bara Asia huku Umoja wa Mataifa ukisema kuwa ni suala ambalo linastahili kuangamizwa kabisa na kutoa wito kwa serikali kulishughulikia kama moja ya haki za wanawake. Rupert Colville ni kutoka ofisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)