Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyota wa Brazili Kaka ahimiza juhudi za UM za kupambana na njaa

Nyota wa Brazili Kaka ahimiza juhudi za UM za kupambana na njaa

Mchezaji hodari wa kandanda wa timu ya Brazil ambaye pia ni balozi mwema wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP, Kaka, amewaomba mashabiki watakao tanzama Kombe la dunia litakalo fanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini kuchangia katika juhudi za kupunguza tatizo la chakula.

Katika tangazo jipya la televisheni, Kaka amewaambia nyoto wa soka kuwa mmoja kati ya watu sita ulimwenguni wanakumbwa na upungufu wa chakula, na wengi wao ni watoto.

Akiwa amebeba kikombe cha plastiki cha rangi nyekundu amewaambia mashabiki kuwa nao pia wanaweza kuchangia katika kupambana na upungufu wa chakula.