UM umezindua mpango kukabiliana na unyanyapaa kwa wenye HIV

8 Juni 2011

Umoja wa Mataifa leo Juni 8 umezindua mpango maalumu wa kukabiliana na unyanyapaa kwa wafanyakazi wanaoishi na virusi vya HIV katika mada ya “unyanyapaa unachagiza maambukizi zaidi”.

Kampeni hiyo pamoja na kuzinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York ambako wakuu wan chi na wawalikishi kutaoka mataifa zaidi ya 30 wanakutana kwa siku tatu kujadili hatua zilizopigwa na zipi mpya zichukuliwe katika vita vya ukimwi pia imezinduliwa katika ofisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa kote duniani.

Lengo kubwa ni kuhakikisha unyanyapaa unatokomezwa kabisa katika sehemu za kazi kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaoishi na virusi na wafanyakazi wengine wote kote duniani.

Emmanuel Mzirai ni mfanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na ukimwi UNAIDS ofisi ya Dar eslamaam Tanzania amezungumza na mwandishi wetu George Njogopa kuhusu kampeni hii na umuhimu wake lakini kwanza anaeleza shughuli zake.

(MAHOJIANO NA MZIRAI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter