Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kusiwe na vuzuizi kwenye matumizi ya mtandao:UM

Kusiwe na vuzuizi kwenye matumizi ya mtandao:UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya haki ya kujieleza Frank La Rue amesema kuwa serikali zilizo na hofu zinaendelea kuweka vizuizi kwenye matumizi ya mtandao kutokana na uwezo wake ya kuwaunganisha watu kuzipinga.

Akiwasilisha ripoti yake mpya kuhusu haki ya kujieleza mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa bwana La Rue amesema kuwa katika miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la idadi ya watu sehemu mbali mbali duniani wanaotaka kuwepo mabadiliko.

La Rue amesema kuwa inastahili kuwa na vizuizi vichache mno katika matumizi ya matandao inapolazimu kuchukua hatua kama hizo kulingana na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Ameongeza kuwa mwaka 2010 zaidi ya watu 100 wanaotumia mtandao walifungwa huku kujieleza kupitia mtandao kukiharamishwa.