Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watunza sera wapata nafasi ya kubaini mafanikio yaliyopo katika matumizi ya nishati ya mimea: FAO

Watunza sera wapata nafasi ya kubaini mafanikio yaliyopo katika matumizi ya nishati ya mimea: FAO

Huku matumizi ya kawi ya mimea yakiendelea kuongezeka shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linazidi kuunga mkono njia mpya zitakazowasaidia watunza sera kuelewa manufaa ya kuwekeza katika sekta hii.

 Mpango huo ulikamilika baada ya majaribio ya miaka mitatu ambapo ulitumika nchini Peru, Tanzania na Thailand. Mkuu wa idara ya FAO inayohusika na matumizi ya nishati ya mimea na usalama wa chakula Heiner Thofern anasema kuwa lengo lao kuu ni kuwasaidia watunza sera kufanya uamuzi ulio bora iwapo nishati ya mimea na hatua mawafaka na kubuni njia ya kupatikana kwa mafanikio zaidi na kupunguza athari zilizopo.

Kupanda kwa bei ya mafuta na hofu ya kuongezeka kwa gesi zinazochafua mazingira vimekuwa vichocheo vya kutumika kwa nishati ya mimea.