Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-Habitat imetoa ripoti kuhusu makazi na mabadiliko ya hali ya hewa

UN-Habitat imetoa ripoti kuhusu makazi na mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT leo limezindua ripoti kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York kuhusu makazi ya binadamu na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti hiyo “Cities and climate change” inatathimini uhusiano uliopo baina ya ukuaji wa miji na mabadiliko ya hali ya hewa, vitu viwili ambavyo ni changamoto kubwa inayoikabili dunia katika karne hii ya 21, ambayo athari zake zina hatari kubwa.

Ripoti hiyo inafafanua mchango wa miji kwa mabadiliko ya hali ya hewa , huku ikieleza athari za mabadiliko hayo kwa wakazi wa mijini. Pia inapitia sera, mikakati na hatua zinazochukuliwa mijini kukabiliana na hali hiyo , ikiwa ni pamoja na mafanikio na vikwazo, mkurugenzi mkuu wa UN-HABITAT Dr Joan Clos anafafanua baadhi ya mabadiliko yanayohitajika

(SAUTI YA DR JOAN CLOS)

Ameongeza kuwa miji inazalisha asilimia 70 ya gesi za viwandani , wakati ipo katika asilimia mbili tuu ya uso wa dunia, hivyo ina wajibu mkubwa wa kukabili gesi hiyo, jambo ambalo serikali nyingi hazilitilii mkazo.