Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD kusaidia nchi masikini kutokuwa tegemezi wa bidhaa

UNCTAD kusaidia nchi masikini kutokuwa tegemezi wa bidhaa

Mawaziri, wanauchumi, maafisa wa serikali na wataalamu wamekutana Jumapili mjini Istanbul Uturuki sambamba na mkutano wa nchi masikini kujadili mipango ya kuzisaidia nchi hizo kujikwamua kutokana na kuegemea bidhaa za chakula na mali ghafi za viwandani kutoka nje.

Utegemezi huo umezifanya kuwa katika hali mbaya zaidi hasa kutokana na mambo yanayoikumba dunia hivi sasa kama matatizo ya karibuni ya chakula, bei za mafuta na mdororo wa kiuchumi.

Mkutano huo umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya uchumi na biashara UNCTAD na mfuko wa pamoja wa masuala ya bidhaa. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)