Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walionusurika waelezea ajali ya boti pwani ya Libya

Walionusurika waelezea ajali ya boti pwani ya Libya

Baadhi ya wahamiaji waliookolewa na kupelekwa kwenye kisiwa cha Lampedusa Italia mwishoni mwa wiki wanasema wameshuhudia boti iliyokuwa na watu kati ya 500 na 600 ikielea kwenye pwani ya Libya mwishoni mwa wiki na maiti zikisukumwa na maji hadi ufukweni.

Taarifa za kuongezeka kwa ajali za boti kwenye bahari ya Mediteraniani zinazidi wakati huu maelfu ya wahamiaji wakijaribu kwa kila njia kukimbia machafuko yanayoendelea Libya.

Mwanamke mmoja wa Kisomali aliyenusurika ameliambia shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwamba boti yao ilizama Ijumaa iliyopita akapoteza mtoto wake na kulazimika kuogelea hadi pwani na ndipo akapata boti nyingine iliyomfikisha Lampedusa.

IOM inasema ingawa watu walishuhudiwa wakiogelea kwenda pwani idadi kamili ya walionusurika haijulikani. Jumbe Omari Jumbe wa IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)