Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufaransa yaainisha vipaumbele vya mkutano wa UNCTAD

Ufaransa yaainisha vipaumbele vya mkutano wa UNCTAD

Ufaransa ambayo ni mwenyekiti wa kundi la nchi 8 zilizoendelea kiviwanda imetaka kuwekwa kwa mipango madhubuti itayohakikisha ulimwengu unaondokana na kitisho cha ukosefu wa chakula.

Akizungumza kwenye mkutano wa UNACTAD, Waziri wa mashirikiano wa Ufaransa Henri de Raincourt amesema kuwa jambo la msingi linalopaswa kuzingatiwa na jumuiya za kimataifa wakati huu ambapo imetoka kwenye mkwamo wa kiuchumi ni kutoyapa kisoga masuala yanayohusu uimarishwaji upatikanaji wa chakula kwani hilo ndilo hitajio kubwa kwa nchi maskini.

 

Ufaransa ambayo pia inaongoza kundi la nchi zinazochipukia kiuchumi G-20 imetaja vipaumbele vyake ikiwemo pia kuweka msukomo wa pekee ili kusaidia maendeleo ya nchi za dunia ya tatu.

 

Imezungumzia suala la chakula, nishati, malighafi na kuzorota kwa uchumi kuwa ni mambo ambayo yaliyotamalaki, hivyo lazima kuwepo kwa juhudi za pamoja kukabiliana na hali hiyo.