Wakulima Ivory Coast wanahitaji msaada:FAO

18 Aprili 2011

Wakati amani inaanza kurejea nchini Ivory Coast baada ya miezi kadhaa ya machafuko ya kisiasa, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO linasema sasa vita vilivosalia ni vya kuokoa mfumo wa kilimo nchini humo.

FAO inasema juhudi zinahitajika kunusuru kilimo cha mpunga na mahindi sasa wakati msimu wa mvua za masika umeanza Magharibi na Kaskazini mwa nchi hiyo.

FAO inasaidia kugawa mbegu, vifaa vya kilimo na mbolea kwa wakulima takribani 12,000 nchini Ivory Coast na Liberia hasa katika vijiji vinavyohifadhi wakimbizi na wakimbizi wa ndani. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud