Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji waliokwama Misrata wako katika hali mbaya:IOM

Wahamiaji waliokwama Misrata wako katika hali mbaya:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema linahofia hatma ya wahamiaji takribani 6000 waliokwama mjini Misrata Libya katika hali mbaya.

IOM inasema hivi sasa boti yake iko njia kuelekea mjini humo kwa lengo la kuwaokoa idadi kubwa ya wahamiaji hao kadri itakavyowezekana. Baada ya wiki kadhaa za kuishi katika maeneo ya wazi, bila chakula cha kutosha, bila maji safi huku wakighubikwa na woga, imearifiwa kwamba wahamiaji hao sasa wako katika hali mbaya kiafya huku wengi wakiwa wamedhoofu na kuwa na upungufu wa maji mwilini.

Kwa mujibu wa IOM theluthi mbili ya wahamiaji hao ni Wamisri, na kundi lingine kubwa la Wanaigeria, Wabangladesh, Waghana, Wasudan, Wairaq, Watunisia na kutoka Niger. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)