Usalama wa watu na maisha yao duniani ni muhimu sana kwa maendeleo na amani:UM
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili umuhimu wa masuala ya usalama wa watu duniani.
Kwa mujibu wa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro usalama wa binadamu unatoa fursa ya kuchukua mtazamo thabiti wa kushughulikia matatizo makubwa na ya aina mbalimbali yanayowakabili watu na jamii zao duniani hivi leo.
Bi Migiro amesema katika mkutano wa kimataifa wa 2005 viongozi wa dunia waliafiki kwamba usalama wa binadamu unagusa mambo mawili muhimu ambayo ni uhuru wa kutoogopa na uhuru wa kutohitaji, lengo ambalo bado linafanyiwa kazi na kila nchi mwanachama kuhakikisha linafikiwa.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa usalama wa binadamu mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya usalama wa watu umesaidia miradi karibu 200 katika nchi 70 duniani. Na amesema kila siku Umoja wa Mataifa unachukua hatua kukabiliana na matatizo ya kiusalama yanayowakabili watu.
(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)