Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna msamaha kwa ukatili wa kimapenzi:Wallstrom

Hakuna msamaha kwa ukatili wa kimapenzi:Wallstrom

Baraza la usalama limetakiwa kuhakikisha kwamba wanaotekeleza ukatili wa kimapenzi kama ubakaji hawapewi msamaha katika makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano Libya au ivory Coast.

Wito huo umetolewa na Margot Wallstrom mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi. Bi Wallstrom amelikumbusha baraza la usalama kuhusu azimio lililopitishwa mwaka 2008 kushughulikia wanawake katika mazingira ya vita.

(SAUTI YA MARGOT WALLSTROM)

Mtakumbuka kwamba azimio 1820 linadai usitishwaji mara moja wa vitendo vyote vya ukatili wa kimapenzi dhidi ya raia kwa pande zote zinzoshiriki vita, na kusisitiza kutolewa uhalifu wa aina hiyo katika msamaha. Pia nalitaka baraza la usalama kutumia ushawishi wake kuhakikisha kwamba makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano Libya au Ivory Coast pia yatajumuisha kusitisha utumiaji wa ukatili wa kimapenzi kama mbinu za vita.