Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara kuanza kuimarika 2011 WTO

Biashara kuanza kuimarika 2011 WTO

Hata baada ya ulimwengu kushuhudiwa kuimarika kwa biashara kwa silimia 14.5 mwaka uliopita huenda pia mwaka huu ukawa na manufaa baaada ya kutabiriwa kuimarika kwa biashara kwa asilimia 6.5 .

Mkurugenzi wa shirika la biashara dunini WTO Pascal Lamy anesema kuwa viwango hivyo vinaonyesha jinsi biashara imeusaidia ulimwengu kuepukana na hali ngumu ya uchumi mwaka 2010. Lammy amesema kuwa ni lazima nchi wanachama wa WTO kuwa makini na kukabilina na changamoto zikiwemo za ukosefu wa ajira kwenye nchini zilizostawi na katika kubuni masoko.

Mwaka 2011 wanauchumi watakuwa wakilenga zaidi katika kuimarika kwa biashara kwa asilimia 6.5 hata kama kuna utata kuhusu athari itakayosababishwa na masuala kadha yakiwemo majanga ya tetemeko la ardhi na tsunami nchini Japan.