Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO kuandaa mkutano wa maendeleo ya sayansi Afrika

UNESCO kuandaa mkutano wa maendeleo ya sayansi Afrika

Shirika la elimu , Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linatarajiwa kuandaa mkutano wa kimataifa kuanzia tarehe 14 hadi 15 mwezi huu mkutano ambao utasisitiza umuhimu wa kuimarisha sayansi na kuzuia kuhama kwa wataalamu kutoka bara la Afrika.

Mkutano huu ambao utawaleta pamoja wanasiasa na wanasayansi mashuhuri pia utaiunga mkono taasisi ya sayansi ya uhasibu nchini Senegal ambayo itapokea wanafunzi wake wa kwanza mwezi Septemba mwaka huu.

Mkutano huo upia utatoa fursa ya kuwasilisha sera kadha zinazochangia kuimarika kwa sayansi barani Afrika.

Wanaotarajiwa kuzungumza kwenye mkutano huo ni pamoja na mshindi wa tuzo la amani katika masuala ya udaktari Françoise Barré-Sinoussi, mjumbe wa Senegal kwenye shirika la UNESCO Papa Momar Diop miongoni mwa wengine.