Skip to main content

Mkuu wa UNHCR akamilisha ziara Misri na kuelekea Kenya

Mkuu wa UNHCR akamilisha ziara Misri na kuelekea Kenya

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres amekamilisha ziara yake nchini Misri ambapo alikagua hatua zilizochukuliwa na shirika hilo katika kushughulikia hali iliyosababishwa na mapigano nchini Libya.

Guterres amesema kuwa hali nchini Libya inastahili kupewa kipaumbele kwa kuwa huenda maelfu ya watu wamekwama kwenye sehemu zinazokumbwa na mapigano. Kwa sasa Guterres yuko nchini Kenya ambapo atazuru kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyo makao ya zaidi ya wakimbizi 320,000 kutoka Somalia.

UNHCR inasema kuwa kuna msongamano mkubwa wa wakimbizi kwenye kambi hiyo kufuatia kuendelea kuwasili kwa wakimbizi zaidi.