Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM wa masuala ya kibinadamu kwa ajili ya Libya anazuru tunisia

Mratibu wa UM wa masuala ya kibinadamu kwa ajili ya Libya anazuru tunisia

Mratibu wa maswala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya ameianza leo ziara ya siku tatu nchini Tunisia.

Mratibu huyo Abdelilah al-Khatib, anakwenda Tunisia kwa lengo la kufanya makadirio ya hali ya kibinaadamu nchini humo na kuzungumza na wakuu serikalini pamoja na wadau wa maswala ya kibinadamu. Hadi sasa kwa uchache watu laki nne na Elfu tano mia moja na saba wameitoroka Libya na kuchukua hifadhi nchini Tunisia .

Kati ya hao Elfu 83 wamerejea nchini Libya mwishoni mwa mwezi machi. Watu wengine 12700 bado wanahitaji msaada wa dharura wakiwa bado wamejazana katika mipaka ya Libya. Fedha Milioni 160 za dola ndizo zinazohitajika kuwasaidia waathirika wa vita , lakini hadi sasa ni asilimia 70 pekee zimepatikana ikiwa ni sawa na milioni 111 za dola.

Shirika la Ocha limesema kwamba Umoja wa Mataifa umekuwa tayari kushirikiana na wafadhili kutafuta msaada huo. Tume ya kibinaamu ya Umoja wa Matifa iko tayari kuelekea Libya ,hata hivo haijapata dhamana za kiusalama.