Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usambazaji chakula wa WFP nchini Libya washika kasi

Usambazaji chakula wa WFP nchini Libya washika kasi

Shughuli za kusambaza chakula nchini Libya kupitia kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP zimewafikia zaidi ya watu 7000 ambao wamehama makwao kutoka mji wa Ajdabiya.

Zaidi ya watu 20,000 wengine walioukimbia mji huo wanatarajiwa kupokea chakula hicho siku chache zijazo. WFP kwa ushirikiano na shirika la mwezi mwekundu pia watagawa chakula kwa watu 85,000 kwa muda wa wiki mbili zijazo kwenye mji wa Benghazi na maeneo yaliyo karibu.

Hao ni watu ambao mara nyingi wanategemea chakula kinachosambazwa kupitia kwa mfumo wa serikai jinsi anavyoeleza Emilia Casella kutoka WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)