Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko makubwa yaendelea kuikumba Namibia:OCHA

Mafuriko makubwa yaendelea kuikumba Namibia:OCHA

Hali ya hatari imetangazwa nchini Namibia baada ya maeneo ya kaskazini nchini humo kukumbwa na mafuriko makubwa.

Kulingana na shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA watu 62 wameuawa kutokana na mafuriko hayo huku zaidi ya vituo 20 vya afya vikiwa vimefurika na mashule 163 kufungwa.

 Kunatarjiwa kutokea mafuriko zaidi kwenye bonde la Cuvelai mwishoni mwa juma baada ya mvua kubwa kutabiriwa kunyesha. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)