Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa wito wa kutozuia fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wanaohitaji Libya

UM umetoa wito wa kutozuia fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wanaohitaji Libya

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Abdel Elah Al-Khatib ameitaka serikali ya Libya kuruhusu bila pingamizi mashirika ya Umoja wa Mataifa ili yaweze kusaidia mamilioni ya Walibya na kuwapa msaada wanaouhitaji.

Bwana Khatib na ujumbe wake wamewasili mjini Tripol jana Jumatatu katika ziara yao yenye lengo la kusaidia kusitisha machafuko kwenye taifa hilo la Afrika ya Kaskazini na kuhakikisha raia wanalindwa.

Katika mkutano wake na katibu mkuu wa kamati ya masuala ya kigeni na ushirikiano wa kimataifa, waziri wa mambo ya nje Moussa Koussa, mwakilishi huyo amerejea wito wake kwa serikali , wito uliotolewa pia na Katibu Mkuu Ban Ki-moon na baraza la usalama wa kukomesha mara moja machafuko yanayoendelea.