Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Ivory Coast yahatarisha maisha ya wakimbizi:UNHCR

Mapigano Ivory Coast yahatarisha maisha ya wakimbizi:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linaendelea kukabiliwa na ugumu kwa kufikisha msaada kwa wakimbizi wa ndani mjini Abidjan kwa sababu ya matatizo ya usalama na fursa ndogo ya masuala ya kibinadamu.

UNHCR na washirika wake hadi sasa wamefanikiwa kuwafikia zaidi ya wakimbizi wa ndani 10,000. Inakadiriwa kuwa watu 300,000 wamekuwa wakimbizi wa ndani mjini Abidjan.

Na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kufuatia mapigano yanayoendelea raia wa Ivory Coast na wahamiaji wanaendelea kuikimbia nchi hiyo, kama anavyofafanua Jemini Pandya kutoka IOM.

(SAUTI YA JEMINI PANDYA)