Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu kwa wanaokimbia Libya yaongezeka:UNHCR

Hofu kwa wanaokimbia Libya yaongezeka:UNHCR

Mapigano yakiongezeka nchini Libya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linahofu kwamba watu wanaotaka kukimbia vita na kutafuta hifadhi hawawezi kuondoka au wanazuiwa kuondoka.

UNHCR inasema imekuwa ikitarajia kuona kundi kubwa la majeruhi hasa wanawake na watoto lakini ni watu wachache tuu waliovuka mpaka, na imeongeza kuwa bado inahofia hali ya wahamiaji wa Kiafrika walioko Libya, na imearifu kwamba wakimbizi wa Eritrea wanashikiliwa kwenye upande wa Mashariki na Magharibi mwa Libya. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

Ameongeza kuwa hadi sasa kuna watu 3500 waliokwama kwenye mpaka wa Libya wengi wao wakiwa ni Wabangladesh. Kundi la Wasomali 35, Waeritrea 5 na Waethiopia watatu waliokuwa wamekwama Benghazi wamesafirishwa kwa boti hadi Alexandria Misri na kisha kupelekwa Saloum na kundi lingine limesafirishwa jana usiku.