Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yakaribisha ahadi ya Misri kuheshimu jumuiya za wafanyakazi

ILO yakaribisha ahadi ya Misri kuheshimu jumuiya za wafanyakazi

Mkurugenzi wa shilika la kazi duniani ILO leo amekaribisha tamko lililotolewa na wa kazi wa Misri kwamba jumuiya za wafanyakazi zitaorodhoshwa na kuruhusiwa kufanya kazi kwa uhuru na ameahidi msaada wa ILO katika kuboresha hali na mazingira ya kazi nchi humo.

Bwana Juan Somavia akihitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Misri amesema ukweli kwamba wizara za fedha na kazi kulialika shirika la ILO kushirikiana nao ni ishara muhimu katika mabadiliko ya sera ,hasa kwenye masuala kama uhuru wa kujumuika, masuala ya mishahara, kulindwa katika jamii na ajira hususan kwa vijana .

Ameongeza kuwa ILO inatiwa moyo na hamasa na juhudi zinazojitokeza katika nchi hiyo hivi sasa. Somavia amezuru Misri kwa mwaliko rasmi wa waziri wa fedha wa Misri Samir Radwan na yule wa ajira na uhamiaji Ahmed El Borai.

Akiwa nchini humo pia amekutana na waziri mkuu Essam Sharaf, maafisa wengine wa serikali, wawakilishi wa jumuiya huru zawafanyakazi, viongozi wa vijana na jumuiya za kijamii. ILO imesema itaisaidia Misri kuunda nafasi za ajira, na pia kuandaa mswada wa sera za kima cha chini cha mishara na kuanzisha miradi ya maendeleo itakayotoa ajira kwa watu wengi.