Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua ofisi kuzisaidia nchi za Afrika ya Kati

UM wazindua ofisi kuzisaidia nchi za Afrika ya Kati

Umoja wa mataifa leo umefungua ofisi maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo wa

kisiasa kwa kuimarisha hali ya amani na kuzua uwezekano wa kutokea machafuko

katika nchi za afrika ya kati.

Ofisi hiyo pia itakuwa na jukumu la kukabiliana na changamoto kwenye maeneo ya mipakani ambako kuna wimbi kubwa la usafirishaji wa magendo wa silaa pamoja na magenge ya uhalifu.

Akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa ofisi hiyo mjini Libreville, Gabon, mwakilishi wa Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya siasa B. Lynn Pascoe amesema kuwa kilio cha muda mrefu kutoka kwa serikali za eneo hilo sasa kimepatiwa

ufumbuzi.

Ofisi hiyo inayojulikana kama UNOCA itafanya kazi kwa muda wa miaka miwili na mwakilishi wake anatazamiwa kuteuliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon.