Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetenga dola milioni 5 kuwasaidia wanaokimbia Libya

UM umetenga dola milioni 5 kuwasaidia wanaokimbia Libya

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ametenga dola milioni tano kuanza juhudi za kuwasaidia watu wanaokimbia machafuko nchini Libya.

Mkuu huyo Valerie Amos amesema watu takribani 147,000 wengi wakiwa ni wafanyakazi wahamiaji wamekimbia machafuko Libya.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky Umoja wa Mataifa na washirika wake wanashirikiana kwa karibu na serikali ya Misri, Tunisia na Niger ili kukidhi mahitaji ya lazima ya idadi kubwa ya watu wanaokimbia Libya. Fedha hizo zitatumika kuongeza juhudi za operesheni za misaada kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia.