Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM uko tayari kusaidia kipindi cha mpito Misri

UM uko tayari kusaidia kipindi cha mpito Misri

Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kusaidia kipindi cha mpito cha kisiasa na kiuchumi nchini Misri.

Nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini inakabiliwa na kipindi cha mabadiliko makubwa baada ya maandamano ya nchi nzima kumlazimisha Rais Hosni Mubarak kujiuzulu.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika masuala ya siasa Lynn Pascoe amekuwa Misri kushudia hali halisi na anasema Umoja wa Mataifa unaweza kutoa msaada wa kiuchumi na kisiasa.

(SAUTI YA LYNN PASCOE)