Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasafirisha wahamiaji wanaokimbia machafuko

IOM yasafirisha wahamiaji wanaokimbia machafuko

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM leo limeanza kuwasafirisha maelfu ya wahamiaji wanaokimbia machafuko nchini Afrika Kaskazini.

Katika siku hii ya kwanza limewasafirisha wahamiaji 900 wa Kimisri kutoka Tunisia hadi Misri kwa kutumia ndege ndogo tano na wengine 900 watasafirishwa kesho Machi mosi.

IOM pia inawasafirisha kundi la wahamiaji 361 wa Bangladesh na 174 wa Mali kutoa Tunisia hii leo huku kukiwa na minpango ya kuwasafirisha wahamiaji zaidi siku ya Jumanne. George Njogopa ana ripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)