Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahofia silaha zinazoingia Ivory Coast kutoka Belarus

Ban ahofia silaha zinazoingia Ivory Coast kutoka Belarus

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amebaini kwa masikitiko na hofu kubwa kwamba helkopta tatu za kivita na vifaa vingine kutoka Belarus vimearifiwa kupelekwa Yamoussoukro kwa ajili ya majeshi ya Laurent Gbagbo.

Vifaa vya kwanza vimearifiwa kuwasili kwa ndege iliyotua Jumapili jioni na ndege zingine zimeripotiwa kuwasili leo Jumatatu. Ban amesema huu ni ukiukaji mkubwa wa vikwazo vya silaha dhidi ya Ivory Coast ambavyo viliwekwa tangu 2004.

Ukiukwaji huo umeripotiwa tayari kwenye kamati ya baraza la usalama inayohusika na vikwazo dhidi ya Ivory Coast. Ban amesema anatumaini baraza la usalama litafikiria kuitisha kikao cha dharura kujadili suala hilo.