Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yataka wanaoondoka Libya wasaidiwe

UNHCR yataka wanaoondoka Libya wasaidiwe

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ameelezea hofu yake juu ya maelfu ya wakimbizi na raia wa kigeni ambao huenda wamekwama nchini Libya.

Amesema hakuna ndege wala boti za kuwasafirisha watu wanotoka maeneono ya vita au nchi masikini walioko Libya na ameezitaka serikali kufikiria haja na mahitaji ya watu hao na sio raia wao tuu.

Amesema wengi wa watu hawa wanahisi wanalengwa, hawana chochote na wanaogopa na kuhofia maisha yao. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)