Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanza kusukuma mbele agenda ya ustawi wa kijamii

UM waanza kusukuma mbele agenda ya ustawi wa kijamii

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umeanza kuweka mipango ya awali ambayo

itahakikisha ustawi wa kijamii unakuwa salama kwa kuwekea vipaumbele maeneo ya

usalama wa chakula, huduma za afya na malipo ya pension.

Maafisa wa Umoja huo wamesisitiza kuwa vipengele hivyo hajipewa uzito kwa muda mrefu kutokana na kukosekana kwa utashi wa kisiasa ili kuvipa msukumo unaostahili.

 

Umoja huo wa mataifa umesema kwamba ustawi wa kijamii ni tunda linalohusika moja kwa moja na haki za binadamu hivyo hakuna njia nyingine wakati huu mbali ya kuanza kulipa kipaumbele.

 

Katika hatua nyingine maafisa wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO wameonya kuwa bila kuwepo kwa misingi dhabiti ya uwekezaji kwenye maeneo ya afya na lishe

ndoto ya ukuzaji uchumi kamwe haiwezi kutokea.

 

Michael Cichon wa ILO, amesema kuwa idadi kubwa ya watu wameendelea kuishi maisha ya kubahatisha huku wakikosa  ubora wa huduma za kijamii