Misaada ya dharura yaanza kuwasili Misri:ICRC

Misaada ya dharura yaanza kuwasili Misri:ICRC

Huku ghasia zikiendelea kushuhudiwa nchini Misri na idadi ya majeruhi kuongezeka ndege ya kwanza ya kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC inayobeba msaada ya dharura ya vifaa vya matibabu imewasili mjini Cairo .

Vifaa hivyo vitatumiwa kuwasaidia watoa huduma ya kwanza katika juhudi zao za kuwatibu watu waliojeruhiwa na vinakadiriwa kuwa vinaweza kuwatibu karibu watu 2000 walio na majeraha madogo na wengine 100 walio na majeraha mabaya.

Kiongozi wa ujumbe wa ICRC mjini Cairo Eric Marclay anasema kuwa lengo lao ni kuwasaidia watoa huduma za kwanza katika juhudi zao za kuokoa maisha akiongeza kuwa wanasafirisha misaada zaidi katika siku zijazo . George njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)